Wakazi wa Karbala wanaomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.
Kiongozi wa maukibu Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Riyaadh Salmani amesema kuwa “Watu wa Karbala wamezowea kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam hadi siku ya mwezi kumi na saba, ambayo ni siku ya saba toka kuuwawa kwake (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Uombolezaji wa watu wa Karbala ni jambo la kitamaduni ambalo wamerithishana vizazi na vizazi, huenda kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maukibu imeanza matembezi upande wa hema hadi kwenye haram ya Husseiniyya, wakapita katikati ya haram mbili tukufu hadi kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) huku wakiimba qaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi.