Wakazi wa nyumba za Abbasi wameomboleza siku ya saba tangu alipouwawa Imamu Hussein (a.s).

Wakazi wa nyumba za Abbasi (a.s) wameomboleza siku ya saba tangu kuuwawa kishahidi Imamu Hussein (a.s).

Kiongozi wa wakazi hao Sayyid Haidari Majhuul amesema “Idara ya wakazi wa nyumba hizi imefanya Majlisi ya kuomboleza siku ya saba tangu kuuwawa kishahidi Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake, imehudhuriwa na kundi kubwa la watu”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imekuwa ikisaidia mawakibu za waombolezaji bila kuchoka, hususan zinazofanywa katika makazi ya Abbasi (a.s)” akasema kuwa “Majlisi za kuomboleza zilianza toka siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam na bado zinaendelea hadi sasa”.

Akaendelea kusema kuwa “Majlisi inavipengele tofauti katika kuomboleza msiba huo, kuna usomaji wa qaswida za husseiniyya, kuwasha mishumaa na mengineyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: