Chuo kikuu cha Al-Ameed katika Atabatu Abbasiyya kimehitimisha semina ya utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi kwa wanafunzi 400 kutoka vyuo tofauti vya Iraq.
Mmoja wa wakufunzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Amiri Twaaiy amesema “Walimu tofauti wa vyuo vya udaktari na uuguzi wamefundisha katika semina hii yenye wanafunzi 400 kutoka vyuo tofauti vya udaktari na uuguzi hapa nchini.
Akaongeza kuwa “Wamefundishwa mambo tofauti ikiwa ni pamoja na, matatizo ya moyo, shindikizo la damu, majanga ya moto na mbinu za utoaji wa huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka muathirika kwenye kituo cha afya”.
Akaendelea kusema “Semina imedumu kwa muda wa siku mbili ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s), washiriki wa semina hii wanatarajiwa kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), wamefundishwa kwa nadhariyya na vitendo”.