Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya inaendesha program maalum kwa wanafunzi Hamsini wa kike.
Kiongozi wa idara hiyo bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi imeandaa program maalum ya wanafunzi Hamsini kutoka kituo cha Fatuma Zaharaa (a.s) chini ya Maahadi” akabainisha kuwa “Program hii inaendana na huzuni za Ashura na matembezi ya mateka kuelekea Sham”.
Akaongeza kuwa “Program iliyoandaliwa na Maahadi imehusisha kuwaweka wanafunzi katika msikiti wa Kufa ambao ndio sehemu walipokaa mateka wa familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) wakati wakipelekwa Sham, wakiwa na kichwa kitakatifu cha mjukuu wa Mtume (s.a.w.w)”.