Kikosi cha Abbasi (a.s) kinafanya Majlisi ya kuomboleza katika Atabatu Husseiniyya.

Kikosi cha Abbasi (a.s) kimefanya Majlisi ya kuomboleza katika mwezi kumi na nane Muharam kwenye hara ya Husseiniyya takatifu.

Rais wa kitengo cha maelekezo ya kidini Sayyid Hassan Mussawi amesema “Miongoni mwa mfululizo wa majlisi za kuomboleza ni Majlisi ya mwezi kumi na nane Muharam, Majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), kuomboleza kifo chake (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake katika ardhi ya Karbala, sambamba na yaliyojiri kwa mateka”.

Akaongeza kuwa “Kikosi huendelea kufanya Majlisi katika kumi la pili na la tatu la mwezi wa Muharam kwenye Husseiniyya na mikoa tofauti ya Iraq”.

Mzungumzaji alikuwa Muheshimiwa Shekhe Abdullahi Dujaili, ameongea kuhusu Imamu Hussein (a.s) katika nyanja ya ubinaadamu na kimaadili kwenye umma wa kiislamu na utekwaji wa familia yake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: