Majmaa-Ilmi imeanza awamu ya tatu ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza awamu ya tatu ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Katibu mtendaji wa mradi Sayyid Muhammad Ridhwa Zubaidi ameongea mbele ya vyombo vya Habari kuwa “Majmaa imeanza kutekeleza awamu ya tatu ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, baada ya kusimama katika siku za mwezi wa Muharam”.

Akaongeza kuwa “Awamu ya mwisho inahusisha wanafunzi zaidi ya (80) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, huku kukiwa na washiriki wa kisoma cha mmoja mmoja (228) na (15) wa kisomo cha vikundi, maandalizi yote yamekamilika”.

Awamu hii itakuwa na majlisi za Husseiniyya na mihadhara mbalimbali pamoja na mashindano, akasema kuwa awamu ya mwisho itadumu kwa muda wa siku (10).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: