Idara ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na program ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed kitengo cha wasichana.
Kiongozi wa idara hiyo bibi Adhraa Shami amesema “Siku ya pili katika program ya kujenga uwezo tumepata idadi kubwa ya walimu wa shule za Al-Ameed, aidha kulikuwa na ratiba ya kuonyesha filamu yenye anuani isemayo (Ujumbe wa mwanamke katika Maisha), imeonyesha nafasi ya mwanamke katika jamii”.
Akaongeza kuwa “Mkufunzi wa semina hiyo bibi Rajaa Ali ameongelea (Fiqhul-Hayaa), amefafanua mambo ya kifiqhi, kisheria, kimaadili, kiitikadi yanayomuhusu mwanamke”.
Akaendelea kusema “Program imepata ushiriki mzuri, kulikuwa na maswali na michango mizuri kutokana na mada zilizofundishwa katika siku ya pili”.