Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya semina ya udaktari kwa watumishi wake.

Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya udaktari kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Semina hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki kwenye maukibu ya Ummul-Banina (a.s), ambalo hutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru wanaokuja katika mji wa Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Semina imejikita katika kueleza utoaji wa huduma za matibabu kwa mazuwaru sambamba na utoaji wa huduma ya kwanza na uokozi.

Semina hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Mujtaba (a.s) chini ya wakufunzi mahiri wenye uzowefu mkubwa, kwa usimamizi wa mkuu wa idara ya afya katika mkoa wa Misaan Dokta Ghazwani Laami.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: