Mkufunzi wa semina bwana Muhammad Thaair Naswrawi amesema “Semina inalenga kuwaandaa watumishi wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani kutoa huduma ya uokozi katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Semina imejikita katika kubainisha matatizo mengi ya kiafya, kama vile matatizo ya moyo kwa watoto na wazee na namna ya kutumia baadhi ya vifaa-tiba wakati wa utoaji wa huduma ya kwanza”.
Akaendelea kusema “Katika semina hii wamefundishwa namna ya kuamiliana na hali tofauti za waathirika, na maelekezo mengine muhimu kwa mtoaji wa huduma ya kwanza na muokozi”.