Rais wa chuo kikuu cha Somar amesema: Jukwaa la siraji linasaidia kubadilisha mfumo wa ufundishaji kutoka kwenye matumizi ya karatasi na kuhamia kwenye matumizi ya kielektronik.

Rais wa chuo kikuu cha Somar katika mkoa wa Dhiqaar Dokta Aadil Radhi Zarkani amesema kuwa, jukwaa la Siraji linasaidia kubadilisha mfumo wa ufundishaji katika vyuo vikuu kutoka matumizi ya karatasi na kuhamia kwenye matumizi ya kielektronik.

Jukwaa hilo ni moja ya program za kituo cha Alkafeel chini ya Chuo kikuu cha Alkafeel.

Akasema: “Kuonyesha jukwaa la Siraji kwa ugeni kutoka kitengo cha uhusiano mkuu na chuo cha Alkafeel, ni sehemu ya kujenga uhusiano baina ya chuo cha Somar na Atabatu Abbasiyya tukufu” akasisitiza kuwa “Jukwaa linamfumo kamili wa ufundishaji kwa njia ya mtandao”.

Akaongeza kuwa “Vyuo vikuu vinauhitaji wa program za kisasa katika kuendesha shughuli zao, sambamba na mfumo wa mitihani unaoendana na maendeleo ya dunia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: