Idara ya maelekezo ya Dini imehitimisha ratiba ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed.

Idara ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya imemaliza wiki ya kwanza ya ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wa kike wa shule za Al-Ameed.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Adhraa Shami amesema “Idara imemaliza ratiba ya wiki ya kwanza ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu katika Ataba tukufu, ratiba hiyo ilihusisha mihadhara miwili ya Fiqhi na Aqida iliyotolewa na idara ya maswali na majibu ya kisheria”.

Akaongeza kuwa “Mwishoni mwa wiki ya kwanza washiriki wamepewa mtihani kutokana na masomo waliyofundishwa”.

Washiriki wameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mafunzo waliyopewa, wameomba mafunzo hayo yaendelee kutolewa kwa watumishi wengine wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: