Mkanda wa kijani kibichi: Tumechangia kutoa ajira na kuingiza mazao ya kilimo sokoni.

Rais wa kitengo cha mkanda wa kijani kibichi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Naasir Hussein Mut’ibu amesema kuwa, mradi wa kijani kibichi umesaidia kutoa ajira na kuingiza mazao ya kilimo katika soko la Karbala.

Akasema kuwa “Hakika mradi wa kijani kibichi unaotekelezwa kwenye eneo lenye ukubwa wa kilometa (27) kaskazini mashariki hadi kusini magharibi ya mkoa wa Karbala umetoa ajira kwa vijana zaidi ya (500), ajira hizo zimesaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira katika mkoa wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Kilimo cha Zaituni, tende na aina zingine za matunda na mbogamboga ni mazao muhimu yanayolimwa katika mradi huu, kwa lengo la kuingiza katika soko la Karbala na kwenye mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya mazuwaru wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya”.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha mkanda wa kijani kibichi, mradi unamaeneo zaidi ya (22), maeneo manne ni maalum kwa ajili ya kupokea familia za wakazi wa Karbala, aidha kitengo bado kinafanya juhudi ya kuongeza sehemu za kilimo na kuandaa sehemu rasmi za kutembelea na kupumzika kwa wanaopenda kutembelea mradi huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: