Kituo cha utamaduni wa familia kinatoa muhadhara kuhusu afya ya nafsi kwa wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa muhadhara kuhusu nafsi kwa wanafunzi wa hatua ya pili walioshiriki kwenye ratiba ya masomo ya kiangazi kwenye Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake.

Mkuu wa kituo bibi Sara Alhafaar amesema “Muhadhara umetolewa na bibi Salma Hamdi kwa wanafunzi wa sekondari (upili) walioshiriki kwenye semina za majira ya kiangazi zilizotolewa na Maahadi ya Qur’ani idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa “Mhadhiri ameongea kuhusu uwelewa wa kulinganisha na madhara yake katika afya ya nafsi”.

Akaendelea kusema “Kituo hutoa mihadhara elekezi siku mbili katika wiki kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’ani tukufu, mihadhara inalenga kuwajenga wanafunzi katika kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: