Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya kongamano la kuratibu ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka 1445h.
Kongamano limefanywa ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu na kuhudhuriwa na katibu wake mkuu Sayyid Hassan Rashidi Abaiji, katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, marais wa vitengo, wawakilishi wa mawakibu na wawakilishi wa idara ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Karbala.
Kongamano limefanywa ndani ya ukumbi wa Khatamul-Ambiyaa, limejikita katika kuangalia shughuli za mawakibu Husseiniyya zitakazo shiriki kuhudumia mazuwaru wanaokuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini mwaka huu.
Katika kongamano hilo imejadiliwa mikakati iliyotumika miaka ya nyumba na kuhimiza kufuata maelekezo yalitotolewa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kwa kushirikiana na idara ya usalama na idara ya afya katika mkoa wa Karbala, ili kulinda usalama na afya za mazuwaru watukufu.