Kiongozi wa idara ya miti na mapambo amesema “Watumishi wetu wamevuna tende zilizopo kwenye uwanja wa katikati ya Ataba mbili ya Husseiniyya na Abbasiyya”.
Akaongeza kuwa “Eneo la katikati ya haram mbili linamitende (56) ambayo ni sawa na umri wa Imamu Hussein (a.s), tende hizo huvunwa kila mwaka na kuzigawa kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa tabaruku.
Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinajukumu la kutunza miti iliyopo eneo hilo takatifu, hususa mitende na kuvuna matunda yake.