Katika wilata ya Hindiyya… Majmaa-Ilmi imefanya Majlisi ya kuomboleza kwa ushiriki wa wanafunzi wa kuhifadhi Qur’ani.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kwa ushiriki wa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu katika wilaya ya Hindiyya.

Majlisi imeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Haidari Ali, akafuata Amiri Qahtwani kisha ukafuata ujumbe kutoka kwa kiongozi wa Maahadi Sayyid Haanid Mar’abi, akaongea kuhusu misingi inayotokana na vizito viwili vitukufu.

Majlisi ikapambwa kwa tenzi na qaswida za kuomboleza kutoka kwa Sayyid Haidari Dhiyaau, zilizoeleza tukio la Karbala na msiba waliopata Ahlulbait (a.s).

Maahadi ya Qur’ani tukufu hufanya Majlisi kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo, kuanzia mwezi wa Muharam hadi mwezi wa Safar, katika ratiba ya kufikisha ujumbe wa vizito viwili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: