Kitengo cha Dini: Harakati mbalimbali zinafanywa na watumishi wetu ndani na nje ya Iraq.

Rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya amesema kuwa, watumishi wa kitengo chetu wanafanya harakati mbalimbali ndani na nje ya Iraq katika mwezi mtukufu wa Muharam.

Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema kuwa “Kitengo kimeshafanya ratiba nyingi toka siku ya shughuli ya kupandisha bendera ya kuashiria kuingia kwa mwezi wa Muharam, kimekuwa kikifanya Majlisi za kuomboleza ndani ya haram tukufu sambamba na kutuma wahadhiri kwenye mikoa tofauti, huku wengine wakienda hadi nchini Kuweit”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wa kitengo hiki hutembelea mawakibu Husseiniyya ndani ya mkoa wa Karbala, na hutoa nasaha na maelekezo, sambamba na kutoa misaada iliyondani ya uwezo wao katika siku hizi za kujiandaa na ziara ya Arubaini”.

Aidha watumishi wa kitengo cha Dini huendesha swala ya jamaa ndani ya haram tukufu na kujibu maswali mbalimbali kwa mujibu wa Dini tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: