Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaombeleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) kwa kufanya majlisi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Majlisi imeelezea maisha ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s) ambayo ni safari muhimu na tukufu kwa kila kizazi, kinatakiwa kuisoma na kuielewa kwa undani, hususan baada ya tukio la Ashura, Maisha yake yanasomo kubwa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) namna alivyo weza kubainisha baina ya haki na batili”.
Akaongeza kuwa “Mhadhiri wa Majlisi ni Shekhe Hasanaini Khaqaani ataongea kuhusu tabia za Imamu Sajjaad (a.s) na namna alivyoweza kufundisha Dini tukufu kupitia msingi wa (Kuweni walinganiaji msio ongea)” akaangazia baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye kitabu cha Swahifatu-Sajadiyya.
Akabainisha kuwa “Majlisi kuu itafanywa karibu na muda wa swala ya Adhuhuri ndani ya ukumbi wa haram tukufu, itadumu kwa muda wa siku tatu, huku Majlisi nyingine ikifanywa saa kumi na moja jioni”.