Katika mji wa Basra.. Kitengo cha Habari na utamaduni kimeandaa semina kwa kikosi cha maukibu ya tamaduni za mimataifa.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa semina kwa wajumbe wa maukibu ya utamaduni wa kimataifa katika mkoa wa Basra.

Maandalizi ya semina hiyo yamesimamiwa na jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo.

Jumuiya imeandaa semina kwa lengo la kufundisha kundi la vijana na kuwapa uwelewa maalum, mkufunzi wa semina hiyo Sayyid Hussein Riyaadh amesema kuwa “Maukibu ya tamaduni za kimataifa itafanyika Basra wakati wa ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa “Semina inahusisha masomo ya fani ya uhadhiri, wanafundishwa namna ya uwasilishaji na mpangilio wa maneno sambamba na lugha ya muili na mambo mengine ya kielimu, aidha wanaelekezwa namna ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini kwa kizingatia mazingira ya ziara hiyo”. Akasema “Semina imefanywa kwa muda wa siku mbili, asubuhi na jioni”.

Akaongeza kuwa “Mwisho wa semina hiyo, wamefanya mtihani wanafunzi watakao shiriki kwenye maukibu ya tamaduni za kimataifa, kwa ajili ya kupima viwango na uwezo wao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: