Kamati ya maandalizi ya wiki ya Imamu ya kimataifa, imefanya kikao cha kujadili mada zitakazo wasilishwa sehemu ya pili.
Kikao cha leo kimejadili baadhi ya mada zilizopendekezwa kuwasilishwa kwenye wiki ya Imamu, rais wa jumuiya ya kielimu ya Al-Ameed Dokta Riyaadh Twariq Amidi amesema “Tumekubaliana mada zitakazo wasilishwa na zitatangazwa baada ya kupitishwa rasmi na viongozi wa juu”.
Akaongeza kuwa “Mada mbalimbali zimewasilishwa kwenye kikao kutoka taasisi tofauti za kielimu na kufanyiwa uchambuzi yakinifu”
Akaendelea kusema “Leo kamati imechagua mada zitakazo wasilishwa kwenye wiki ya Imamu, zitajadiliwa tena kwenye kikao kijacho kabla ya kutangazwa”.