Kwa kuhudhuria kiongozi wake wa kisheria.. Atabatu Abbasitya imeshiriki katika kongamano la kitabu cha Sajadiyya la kimataifa awamu ya tisa.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amehudhuria kwenye kongamano la kitabu cha Sajadiyya la kimataifa awamu ya tisa, linalosimamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu.

Hafla ya ufunguzi imefanywa chini ya anuani isemayo “Ujumbe wa elimu katika historia na turathi za Imamu Sajjaad (a.s)”, kongamo hilo litafanyika kwa muda wa siku tatu, linapambwa na vikao vya kielimu ndani ya ukumbi wa Khatamul-Ambiyaa (s.a.w.w) katika Atabatu Husseiniyya, aidha kuna maonyesho ya vitabu katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.

Hafla ya ufunguzi imehudhuriwa na viongozi wawili wakisheria kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, Shekhe Abdulmahadi Karbalai na Sayyid Ahmadi Swafi, bila kusahau wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Jawadi Hasanawi, Dokta Abbasi Rashidi Didah Mussawi, wameshiriki pia watafiti kutoka nchi za kiarabu na kiislamu na wawakilishi wa vyuo vikuu vya Iraq.

Ushiriki wa Ataba tukufu unatokana na mualiko kutoka Atabatu Husseiniyya, mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Didah Mussawi amesema kuwa “Kongamano la kitabu cha Sajadiyya la kimataifa awamu ya tisa linafanywa sambamba na kumbukizi ya kifo cha Imamu Sajaad (a.s)”.

Akasema “Kongamano limejikita katika ujumbe wa elimu na nafasi ya Imamu Sajjaad (a.s), Pamoja na kufafanua baadhi ya vifungu vya dua katika kitabu cha Sajadiyya na jinsi vinavyo muunganisha mja na Mola wake, na kueleza nafasi ya wanachuoni katika kuhuisha turathi za maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.

Akasema kuwa “Kitengo cha Habari na utamaduni kitakuwa na ushiriki mkubwa kwenye vikao vya kitafiti, Pamoja na kushiriki kwenye vikao vya ujumbe wa Imamu”.

Rais wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Sayyid Jamali Dili Shahristani amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu inaushiriki maalum kwenye kongamano la kitabu cha Sajadiyya awamu ya tisa, sambamba na ushiriki wake kwenye maonyesho ya vitabu yatakayodumu kwa muda wa siku kumi, itaonyesha machapisho ya kitengo cha Habari na utamaduni kikiwemo kitabu kilichaondikwa na Shekhe Jaasim Karkushi, kitengo cha Habari na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: