Katika mji wa Kirkuut.. Kitengo cha mahusiano kimekamilisha maandalizi ya ufunguzi wa kituo cha kijana wa Alkafeel.

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemaliza maandalizi ya ufunguzi wa kituo cha kijana wa Alkafeel, kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za mkoa wa Kirkuuk.

Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule Sayyid Maahir Khalidi amesema “Watumishi wetu wamekamilisha maandalizi ya ufunguzi wa kituo cha kijana wa Alkafeel, karibu na Maqaam ya Zainul-Aabidina (a.s) katika wilaya ya Daquuq mkoani Kirkuuk, kituo hicho kinafanywa kwa mwaka wa pili mfululizo ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).

Akaongeza kuwa “Tumekamilisha shughuli zote za maandalizi ya kufungua vituo sita vya kielimu na kitamaduni, miongoni mwa vituo hivyo ni kituoa cha kusahihisha usomaji wa surat Fat-ha na kuonyesha filamu ya (Ahmadi na mwezi), kituo cha kuonyesha tukio la Twafu na kituo cha (Soma kitabu na upime nafsi yako)”.

Akaendelea kusema “Shughuli hizi ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya idara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: