Maahadi ya Qur’ani kitengo cha wanawake imefanya shindano la (Lu-u lu-u maknuun) la kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Maahadi ya Qur’ani tukufu kitengo cha wanawake/ tawi la Waasit chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya shindano la (Lu-u lu-u maknuun) la kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa ushiriki wa wanafunzi (48) wa Maahadi.

Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Shindano la Qur’ani linalosimamiwa na Maahadi katika mkoa wa Waasit linamakundi matatu ambayo ni (waliohifadhi juzuu 3, juzuu 5 na juzuu 10)”.

Akaongeza kuwa “Jumla ya washindani walikuwa (48) katika kila kikundi walipatikana washindi watatu”.

Akabainisha kuwa “Maahadi inatoa kipaombele sana cha kufanya mashindano ya Qur’ani kwa ajili ya kuwatia moyo wanafunzi waendelee kuhifadhi na kusoma Dini yao tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: