Kituo cha utamaduni wa familia kinatoa mihadhara elekezi kwa walimu wa shule za Al-Ameed.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa mihadhara elekezi kwa walimu wa shule za Al-Ameed.

Mkuu wa kituo Bibi Sara Hafaar amesema “Kwa ajili ya kujenga uwelewa wa kifamilia katika jamii wa wasichana, kituo cha utamaduni wa familia kinatoa mihadhara elekezi kwa watumishi wa shule za Al-Ameed”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara wa kwanza ulikuwa na anuani isemayo (Kuwasiliana na watoto) kutoka kwa bibi Nabaa Swabaah Haidari, muhadhara wa pili ukawa na anuani isemayo (Siri za kupata amani ya nafsi)”.

Kituo kinaendelea kutoa elimu kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kuhusu mbinu za kupata utulivu katika familia na furaha ya nafsi kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: