Muheshimiwa katibu mkuu ameyasema hayo kwenye kongamano la waandishi wa Habari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, akaongeza kuwa “Tumeandaa mkakati wa matangazo ya ziara ya Arubaini chini ya usimamizi wa moja kwa moja kutoka kwa Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, sambamba na kuitikia maombi ya waandishi wa Habari ya kurusha picha halisi za tukio hili tukufu hapa Iraq na duniani kote”.
Akasisitiza kuwa “Kuangazia semina na warsha za waandishi wa Habari kwenye vitengo tofauti”, akasema “Wanahabari wote wanatoa huduma moja” akasisitiza “Umuhimu wa kutoa elimu ya huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya kwa kufuata mwenendo wa Maimamu watakatifu na misingi ya kibinaadamu”.
Muheshimiwa katibu mkuu akahimiza “Kuzingatia muonekano na heshima ya Atabatu Abbasiyya, kwani imekuwa mstari wa mbele kujenga uhusiano na serikali na kufikisha ujumbe usiokinzana”.