Kufanikiwa kwa upasuaji wa mtoto aliyekuwa na tatizo la kutembea kwa sababu ya ufupi wa mishipa ya miguu.

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kutibu mtoto aliyekuwa na tatizo la kutembea.

Daktari bingwa wa mifupa na majeraha Dokta Bariri Asadi amesema “Kazi ya kurefusha mishipa ya mguu ya mtoto mwenye umri wa miaka saba imefanyika kwa mafanikio, alikuwa na tatizo kwenye ubongo lililosababisha tatizo la mishipa ya kwenye miguu na shida ya kutembea”.

Akaongeza kuwa “Tumefanikiwa kurudisha hali ya kawaida kwa mtoto huyo”. Akasisitiza kuwa “Mafanikio hayo yanatokana na jopo la madaktari bingwa wa Iraq na vifaa-tiba vya kisasa vilivyopo hospitalini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: