Majmaa-Ilmi imeweka kituo cha mahafidhi kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru katika mji wa Najafu.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeweka kituo cha kuhudumia mazuwaru wanaokuja kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) katika mji wa Najafu.

Waratibu wa kituo hicho ni Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Wahudumu ni mahafidhi wa Qur’ani tukufu, wametoa huduma tofauti kwa mazuwaru na waombolezaji wa kifo cha Imamu Ali bun Hussein (a.s) mwezi ishirini na tano Muharam.

Maahadi ya Qur’ani hutilia umuhimu mkubwa kituo hiki kwa ajili ya kuwajenga wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani katika kutumikia vizito viwili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: