Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s) katika ukumbi wa utawala.

Mhadhiri Shekhe Ali Abu Hawatim Twaaiy amesema “Atabatu Abbasiyya hufanya Majlisi za Husseiniyya na kuomboleza vifo vya Ahlulbait (a.s), ikiwemo Majlisi ya leo ambayo tumeomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Tumeangazia mambo mawili muhimu, tumeangazia ibada za Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na nafasi yake katika kuelezea tukio la Twafu”.

Ni kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu kufanya maombolezo ya kumbukumbu za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) mbele ya wahudumu wake na mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: