Maukibu ya watu wa Karbala inaomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).

Maukibu ya watu wa Karbala inaomboleza kifo cha Imamu wa nne miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) Imamu Sajjaad (a.s), katika uwanja wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Mawakibu za kuomboleza, zimeanza matembezi asubuhi ya Jumapili kuelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Waombolezaji wameshindikiza jeneza la kuigiza la Imamu Sajjaad (a.s), wametoa pole kwa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi.

Mawakibu za uombolezaji hufanya hivyo siku ya mwezi ishirini na tano Muharam, ambayo ndio siku aliuwawa Imamu Zainul-Aabidina (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: