Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).

Watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, wanaomboleza kifo cha Imamu Ali Sajjaad (a.s) kwa maukibu ya pamoja.

Maukibu imeanza matembezi yake ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakiimba qaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi katika nafsi za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Maukibu hiyo ilipowasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) ikafanya majlis iliyohudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru na waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: