Hospitali ya Alkafeel imefanikiwa kutibu mtoto aliyekuwa na tatizo la kutembea.

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kutibu mtoto aliyekuwa na tatizo la kutembea.

Daktari bingwa wa mifupa na upasuaji Dokta Bariri Asadi amesema kuwa “Mtoto mwenye umri wa miaka 7 alikuwa na tatizo kwenye ubongo wake lililopelekea tatizo la kushindwa kutembea”.

Akaongeza kuwa “Tumefanya upasuaji kwa umakini wa hali ya juu na tumefanikiwa kurudisha uwezo wake wa kutembea katika hali ya kawaida”.

Akasisitiza kuwa “Mafanikio hayo yanatokana na jopo la madaktari bingwa wa Iraq na vifaa-tiba vya kisasa vilivyopo hospitalini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: