Kitengo cha mahusiano kinaendelea na shughuli za kituo cha kijana wa Alkafeel katika mji wa Kirkuuk.

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea na shughuli za kituo cha kijana mzalendo wa Alkafeel awamu ya pili katika wilaya ya Daquuq mkoani Kirkuuk.

Kituo hicho kinasimamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo na shule chini ya kitengo.

Mkuu wa kituo hicho Sayyid Karaar Hasanawi amesema “Idara inaendelea na shughuli za kituo cha kijana mzalendo wa Alkafeel kwa mwaka wa pili mfululizo, tunatoa huduma za kitamaduni sambamba na kuhudumia mazuwaru wanaokuja kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) kwenye Maqaam yake katika wilaya ya Daquuq”.

Akaongeza kuwa “Kituo kina idara (6) za kitamaduni, kinafanana na vituo ambavyo huwekwa katika mji wa Karbala wakati wa ziara ya Arubaini chini ya harakati ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel”.

Muwakilishi wa mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel katika mji wa Kirkuuk Sayyid Muhammad Zainul-Aabidin amesema “Kituo kina (Idara ya uendelezaji wa vijana), yenye jukumu la kujenga uwezo wa vijana na kuhudumia mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: