Majmaa Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inatoa mihadhara ya kitamaduni kupitia mradi wa Qur’ani.
Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Baabil Sayyid Muntadhir Mashaikhi amesema “Mihadhara hiyo ni sehemu ya mradi wa Qur’ani sambamba na kueleza historia ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) na kizazi chake”.
Akaongeza kuwa “Mihadhara inatolewa kwa muda wa siku mbili mfululizo kwenye vitongoji tofauti vya mkoa wa Baabil”.
Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake tofauti ni moja ya vituo vya Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kueneza elimu ya Qur’ani katika jamii.