Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye warsha ya kuboresha Maisha ya raia wa Iraq.

Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya umeshiriki kwenye warsha yenye anuani isemayo (Mkakati wa kitaifa wa kuboresha Maisha) chini ya kituo cha Nahrain cha tafiti za kimkakati jijini Bagdad.

Muwakilishi wa Ataba kwenye warsha hiyo na makamo wa rais wa kitengo cha maendeleo endelevu Sayyid Haidari Ghazi Khaswafu amesema “Warsha imehusisha wawakilishi kutoka ofisi ya Waziri mkuu wa Iraq na taasisi za kijamii, Atabatu Abbasiyya imekuwa na ushiriki mkubwa kwa kuonyesha miradi ya utoaji wa huduma katika jamii”.

Akaongeza kuwa “Washiriki wote wamewasilisha tafiti zao kwenye sekta hiyo, tafiti ya Atabatu Abbasiyya ilikuwa inasema (Mkakati uliofanikiwa katika Atabatu Abbasiyya wa kuboresha Maisha katika taifa la Iraq)”.

Akafafanua kuwa “Zimetajwa takwimu na matokeo tofauti, miongoni mwa takwimu hizo ni ile ya kutokomeza ufakiri, kuwezesha wanawake, msaada katika sekta ya afya na elimu, usambazaji wa maji safi pamoja na kuelezea miradi ya Ataba iliyopata mafanikio katika kuboresha Maisha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: