Kitengo cha habari na utamaduni kinaomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) nchini Tanzania na Chadi.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimehuisha kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) katika nchi mbili, Tanzania na Chadi kwa kufanya Majlisi za kuomboleza.

Majlisi hizo zimesimamiwa na Markazi Dirasaat Afriqiyya chini ya kitengo.

Mkuu wa kitengo Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Mubalighina wa Markazi katika bara la Afrika wanaendelea kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) kwa kufanya Majlisi za kuomboleza mbele ya wapenzi wa Ahlulbait”.

Mubalighi wa Markazi katika nchi ya Tanzania Shekhe Ammaar Maulid amesema “Majlisi imeeleza tabia na ibada za Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na athari yake katika kurekebisha umma, sambamba na harakati yake (a.s) baada ya kifo cha baba yake Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake watukufu”.

Naye mubalighi wa Chadi Shekhe Ali Muhammad akasema “Majlisi imejikita katika kueleza maadili aliyokuwa nayo Imamu Ali bun Hussein (a.s), hakika alifanya kazi kubwa ya kufundisha Dini tukufu, alipambana na mmomonyoko wa maadili na jamii, sambamba na kupambana na utawala wa bani Umayya uliokua unatishia uhai wa Dini tukufu ya Kiislamu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: