Bendera ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zimepandishwa juu ya mnara wenye urefu wa mita 420 ambao ndio mnara mrefu zaidi jijini Tehran.
Rais wa kamati ya ushauri wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Twalaal Biir amesema “Siku ya Jumanne jijini Teheran imepandishwa bendera ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) Pamoja na bendera ya Atabatu Alawiyya, Kadhimiyya, Askariyya, Zainabiyya na Radhawiyya, kwenye mnara ya Milaad wenye urefu wa mita 420”.
Akaongeza kuwa “Zowezi hilo limefanywa baada ya kamati ya Arubaini ya Imamu Hussein kuialika Atabatu Abbasiyya tukufu kuhushuria shughuli ya kupandisha bendera hizo kwenye mnara huo katika wakati huu wa kuelekea ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akabainisha kuwa “Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeongozwa na Sayyid Hashim Milani, watumishi wa idara ya masayyid na watumishi wa idara ya mahusiano sambamba na watumishi wa Ataba zingine”.