Kitengo cha Dini kinatoa mihadhara kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kinatoa mihadhara elekezi kwa watumishi wa vitengo vinavyo hudumia moja kwa moja mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Wahadhiri ni Shekhe Swalahu Karbalai na Shekhe Ali Mujaan.

Shekhe Mujaan amesema “Kitengo kimejiandaa kupokea idadi kubwa ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kimekuwa kikitoa mihadhara elekezi kwa watumishi wa vitengo vinavyotoa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili ni miongoni mwa vitengo vya kwanza kupata mihadhara elekezi, kwani kitengo hicho kinatoa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru, hivyo watumishi wake wamepewa maelekezo maalum kuhusu ziara za Arubaini”.

Akasema kuwa “Tunaendelea kutoa mihadhara elekezi kwa vitengo vingine pia, sasa hivi tunaelekea kwenye kitengo cha kulinda nidham, kisha tutaenda kwenye kitengo cha utumishi, mihadhara inatolewa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), inawajenga kuwa watumishi bora Zaidi katika siku za ziara ya Arubaini inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: