Idara ya maelekezo ya Dini inaendeleza ratiba ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed.

Idara ya maelekezo ya Dini katika Atabatu Abbasiyya inaendeleza ratiba ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed.

Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema, “Kwa wiki ya pili mfululizo Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeendelea na ratiba ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed ndani ya ukumbi wa Sardabu ya Alqami kwa ushiriki wa walimu (57)”.

Akaongeza kuwa “Ratiba inahusisha mada isemayo (Ujumbe wa mwanamke katika Maisha), imejikita katika kueleza nafasi ya mwanamke katika kulinda misingi ya Dini akitimiza wajibu wake”.

Akaendelea kusema “Bibi Rajaa Ali akaongea mada ya Fiqhi yenye anuani isemayo (Fiqhul-Hayaa) na akajibu maswali kutoka kwa washiriki”.

Idara inatekeleza ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wanaotoa huduma kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: