Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa program ya kitamaduni iitwayo (msimu wa maarifa ya utamaduni) kwa wanafunzi wa sekondari ya Ummu-Habiba.
Mkuu wa kituo bibi Sara Hafaar amesema “Program inafanywa kwa kushirikiana na idara ya malezi ya Karbala, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Vipi nitalinda moyo wangu), kisha kikafuata kipindi cha (picha na maoni) chini ya mkufunzi Sundus Muhammad”.
Akaongeza kuwa “Katika program hiyo kulikuwa na kipengele cha (Kutoka kwenu hadi kwenu) cha kujibu maswali tofauti, kilicho simamiwa na Nabaa Haidari na Sundus Muhammad, halafu ikahitimishwa kwa mtihani wa kitamaduni na kimaarifa uliosimamiwa na Ikhlasu Jawaad na Zaharaa Faaiz”.
Kituo kinatumia wakati wa likizo za kiangazi kutoa mafunzo kwa wanafunzi na kuwajenga waweze kupambana na changamoto za Maisha na familia kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).