Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa kabati 100 zenye masanduku 3000 vya kuhifadhi mali za mazuwaru na kinaendelea kutengeneza sehemu mpya kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.
Kiongozi wa idara ya Amanaati Sayyid Jafari Aali-Taamah amesema “Watumishi wetu wametengeneza kabati 100 zenye sanduku 3000 za kuhifadhi mali za mazuwaru wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Idara inaendelea na kazi ya kukarabati kabati zilizo haribika pamoja na kutengeneza mpya zitakazo tumika kuhifadhi mali za mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq”.
Akaendelea kusema “Idara imeandaa zaidi ya Abaya (1500) za kiislamu kwenye maeneo ya kugawia hijabu, yaliyopo katika Barabara ya Maitham Tamaar karibu na Ataba tukufu wakati wa siku za ziara”.