Maukibu 100 zinatoa kuhuduma kwa mazuwaru wa Arubaini katika kitongoji cha Abu-Khaswibu – Basra.

Zaidi ya maukibu 100 katika kitongoji cha Abu-Khaswibu mkoani Basra zinahudumia mazuwaru wa Arubaini mwaka huu.

Kiongozi wa mawakibu Sayyid Ahmad Jasim Swalehe amesema “Maukibu za kutoa huduma katika eneo la mji wetu hadi Barabara ya Al-ufuud zilizo sajiliwa rasmi zipo zaidi ya 100 zimejipanga pembeni ya Barabara yenye urefu wa (km 35)”, bado kuna Husseiniyya na nyumba nyingi za watu binafsi zimefungua milango na kutoa huduma kwa mazuwaru.

Akaongeza kuwa “Mawakibu zinatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wanaoenda Karbala, ikiwemo chakula, vinywaji, malazi, huduma za afya na zinginezo”.

Akabainisha kuwa “Mawakibu za Husseiniyya katika mji wa Abu-Khaswibu haziishii kutoa huduma tulizotaja peke yake, bali zinasaidia kulinda amani pia, baada ya misafara ya mazuwaru kuisha katika mji huu, wahudumu wa mawakibu nao wataanza kutembea kwa mikuu kuelekea Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: