Marjaa Sistani amepokea wakazi wa kitongoji cha Jadiriyya.

Marjaa Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Sistani, amepokea wakazi wa kitongoji cha Jadiriyya kilichopo mji mkuu wa Bagdad.

Tamko la ofisi yake linasema:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Muheshimiwa Sayyid Sistani leo kabla ya muda wa Adhuhuri amepokea wakazi wa kitongoji cha Jaadiriyya, ambao walionekana kwenye vyombo vya Habari wakilalamika kuwa wanapewa shinikizo la kuondoka kwenye ardhi zao kwa manufaa ya baadhi ya watu.

Muheshimiwa amelaani jambo hilo ambalo ni kinyumbe cha sheria na katiba, akasema miongoni mwa wajibu muhimu kwa wale walio kwenye uongozi ni kulinda mali na haki za raia, na kusimama dhini ya waovu wanaoeneza hofu.

(2/Safar/1445h).

Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: