Kitengo cha mahusiano kimeandaa ratiba ya vijana kutoka Ujerumani.

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa ratiba ya vijana wa kituo cha Husseiniyya-Zaharaa (a.s) kutoka nchini Ujerumani.

Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule Sayyid Maahir Khalidi Almayahi amesema “Idara imeandaa ratiba ya kitamaduni na kidini kwa wageni (34) kutoka kituo cha Husseiniyya-Zaharaa nchini Ujerumani, kuanzia mapokezi yao katika uwanja wa ndege wa Baghdad na kuelekea kufanya ziara katika Atabatu Kadhimiyya na kutoa muhadhara wa kitamaduni na kidini kwa wageni hao”.

Akaongeza kuwa “Ugeni ukaelekea katika mji wa Samaraa kufanya ziara kwenye Atabatu Askariyya na malalo ya Sayyid Muhammad kisha ukaelekea katika mkoa wa Najafu kufanya ziara kwenye Atabatu Alawiyya, Masjid Kufa na Sahala, sambamba na kuhudhuria mihadhara mingi ya kidini na kitamaduni”.

Akaendelea kusema “Ratiba ikahitimishwa kwa wageni hao kukaa katika mji wa Karbala kwa muda wa siku tano, wamefanya ziara katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kutembelea miradi tofauti ya Atabatu Abbasiyya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: