Kitengo cha usafirishaji kimeanza kukarabati gari zake kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini inayohudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kitengo cha usafirishaji katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kukarabati gari zake, kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Makamo rais wa kitengo cha uhandisi Karaar Haidari Abdulkarim amesema “Kitengo kimeanza kufanya ukarabati wa gari zitakazoshiriki kubeba mazuwaru wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), sambamba na gari za maji na wagonjwa”, akasema kuwa ukarabati huu ni sehemu ya kujiandaa na ziara ya Arubaini tukufu.

Akasema “Ukarabati huo unahusisha kuandaa vifaa vya dharura, vinavyoweza kuhitajika wakati wa ziara, sambamba na kuandaa mafuta na mahitaji mengine”.

Kwa mujibu wa Abdulkarim “Kitengo kimeandaa jopo la mafundi litakalokuwa na wajibu wa kutengeneza gari lolote litakaloharibika wakati wa kazi, na kuhakikisha gari zote zinafanya kazi vizuri wakati wote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: