Kitengo cha habari na utamaduni kimepata tuzo kwenye kongamano la kitabu cha Sajaadiyya.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kupitia kituo cha tafiti za kielimu kimepata tuzo kwenye kongamano la kitabu za Sajadiyya la kimataifa awamu ya tisa.

Kongamano limefanywa na Atabatu Husseiniyya kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).

Mkuu wa kituo Shekhe Hassan Jawadi amesema “Tumeshiriki kwenye kongamano hilo tukiwa na kitabu kinachoeleza historia ya Imamu Sajjaad (a.s), Maisha yake, msimamo wake na nafasi yake katika kuelezea harakati ya Imamu Hussein (a.s) na malengo yake”.

Akaongeza kuwa “Tumeshiriki kupitia kituo cha tafiti za kielimu chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kwa kuonyesha kitabu kilichoandikwa na Muheshimiwa Shekhe Jaasim Karkushi, kiitwacho (Sayyid Saajidina: Mfano wa Subira, elimu na kazi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: