Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa ratiba ya kitamaduni kwa watumishi wa Wakfu-Shia katika mkoa wa Kirkuki.
Kiongozi wa idara ya mahusiano ya ndani Sayyid Rasuul Naji amesema “Idara imepokea watumishi wa Wakfu-Shia wakike na wakiume katika mkoa wa Kirkuki”.
Akaongeza kuwa “Ratiba iliyo andaliwa inahusisha kutembelea Ataba mbili tukufu na kuangalia makumbusho ya Alkafeel na nakala-kale sambamba na kusikiliza muhadhara kutoka kwa Shekhe Harithi Dahi”.
Akaendelea kusema “Ratiba imepambwa na kutembelea miradi ya Ataba, kikiwemo kiwanda cha Aljuud, kiwanda cha barafu na vitalu vya Atabatu Abbasiyya tukufu”.