Kitengo kinachohudumia uwanja wa katikati ya haram mbili kimeanza kukarabati gari zake kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Watumishi wanaohudumia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kukarabati gari zao kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Kiongozi wa idara ya mitambo Sayyid Muhammad Abdu Ali Mussa amesema “Watumishi wetu wameanza kufanya ukarabati wa gari kutokana na kukaribia kwa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Tuna gari za kubeba maji safi ya kunywa, chakula na barafu ambazo husambaza vitu hivyo kwa Mawakibu-Husseiniyya, bila kusahau gari za kufanya usafi katika eneo la katikati ya haram mbili na maeneo jirani”.

Akaendelea kusema kuwa “Idara imeandaa gari za hakiba zinazoweza kutoa huduma wakati wowote zikihitajika wakati wa siku za ziara inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: