Atabatu Alawiyya imepokea bendera ya huzuni kutoka Atabatu Abbasiyya.

Atabatu Alawiyya tukufu imepokea bendera nyeusi ya huzuni kutoka Atabatu Abbasiyya kufuatia kumbukizi ya kifo cha Imamu Hassan (a.s).

Makamo rais wa kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Jaluhani amesema “Tumekuja kukabidhi bendera nyeusi inayo ashiria huzuni katika Atabatu Alawiyya chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, kufuatia kukaribia kwa kumbukumbu ya kuuwawa kwa Imamu Hassan (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Hii ni bendera maalum ya mjukuu mkubwa wa Mtume mtukufu Imamu Hassan Almujtaba (a.s) imeandikwa maneno yasemayo (Asalam Alaika yaa Abaa Muhammad Hassan Almujtaba)”.

Naye rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Alawiyya Shekhe Karaar Khafaaji akaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa zawadi hiyo, akasema kuwa “Bendera itapepea kuhuisha msiba wa Aalu Muhammad (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: