Mazuwaru wanaoenda Karbala kuhuisha Arubaini ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) wanaendelea kutembea katika mkoa wa Basra.
Mazuwaru hao wamewasili katika wilaya ya Qarnah kaskazini ya mkoa wa Basra, kutokea kitongoji cha Raasu-Bisha, wanatarajiwa kutembea umbali wa (km 400) takriban hadi wafike Karbala.
Mawakibu zilizo enea kila sehemu zinatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru hao, wakazi wa maeneo wanayopita wamefungua milango ya nyumba zao na kujitolea kila wanachoweza kwa mazuwaru.
Mji wa Basra ndio sehemu ya mbali Zaidi kusini mwa Iraq wanakotoka mazuwaru kwa miguu hadi Karbala, huungana na wakazi wa mikoa mingine ya kusini katika matembezi ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).