Kitemho cha habari na utamaduni chafanya semina ya Aqida na Fiqhi nchini Tanzania.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya semina ya Aqida na Fiqhi katika mji wa Kigoma nchini Tanzania.

Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Markazi imefanya semina ya kidini kuhusu Fiqhi na Aqida katika mkoa wa Kigoma kupitia muwakilishi wetu wa Tanzania Shekhe Abdulhakim Yunusi”.

Akaongeza kuwa “Semina imedumu kwa zaidi ya siku kumi, ilihusisha utoaji wa mihadhara ikiwa ni sehemu ya kunufaika na kipindi cha likizo za shule, na zimehudhuriwa na wapenzi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akasendelea kusema “Misafara ya kitablighi inaendelea kwa lengo la kufundisha uislamu halisi kwenye miji tofauti ya Afrika chini ya usimamizi wa wawakilishi wetu waliopo katika bara la hilo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: